Serikali nchini, imepanga kufumua gridi ya Taifa na kuifanyia marekebisho kutokana na changamoto ya umeme kukatika nchini, mpango ambao ni mahususi utakaosaidia nchi kuzalisha umeme wa kutosha.
Hayo yamebainishwa hii leo Februari 3, 2023 na Waziri wa Nishati, January Makamba wakati akijibu swali bungeni kuhusu umeme akisema, “kukatika niseme tu kwamba tunafahamu na changamoto bado ipo tunakiri.”
Amesema, “lakini ambacho nataka niwahakikishie waheshimiwa wabunge na watanzania hivi tunavyoongea tunayo mipango madhubuti ya kuifumua gridi nzima na kuirekebisha kwasababu changamoto iliyokuwepo ni miundombinu chakavu.”
”Hili jambo ukubali ukatae ndiyo ukweli kwamba miundombinu yetu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme ilikuwa haitoshelezi mahitaji na haijafanyiwa marekebisho muda mrefu” amesema Waziri Mkamba.
Aidha, amefafanua kuwa, ”Februari 15 2023, tunasaini mradi unaitwa gridi imara ni miradi 26 ya takribani trilioni 1 na waheshimiwa wabunge tutawaalika mshiriki kwasababu ni jambo amablo litaenda kuanza safari ya kumaliza changamoto ya miundombinu uzalishaji wa umeme tunaongeza ilitusiwe na gap.”