Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira – NEMC, limepokea na kushughulikia malalamiko 369 ya uchafuzi na uharibifu wa Mazingira, ikiwemo kuvuja kwa mabomba ya mafuta na kuchoma taka hatarishi chini ya kiwango kinachotakiwa kisheria.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC,  Dkt. Samwel Gwamaka ameyasema hayo hii leo Machi 3, 2023 jijini Dodoma, wakati akieleza mafanikio ya Baraza na kusema malalamiko hayo ya Wananchi ni ya kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Februari 2022.

Amesema malalamiko hayo yalihusisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, utiririshaji wa maji taka, uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwandani, kelele za muziki, kushamiri kwa gereji bubu maeneo ya makazi, kushamiri vituo vya mafuta katikati ya makazi ya watu, matumizi ya mifuko ya plastiki iliyokatwa na kutapaka maeneo ya makazi na kusema itahakikisha inatoa elimu sahihi na suluhisho juu ya changamoto hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa NEMC,  Dkt. Samwel Gwamaka.

Aidha, katika hatua nyingine Dkt. Gwamaka amesema Baraza limefanikiwa kusajili miradi 1702 ambapo 967 kati yake ni ya tathimini ya athari za mazingira – TAM na 735 ni ya ukaguzi wa Mazingira.

Aidha, amesema NEMC imetoa Jumla ya Vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya nchi ambapo vibali 10 ni vya uingizaji na usafirishaji nje ya nchi na kupelekea kiasi cha tani 516,041 za taka mbalimbali kukusanywa na makampuni yenye vibali.

“kukusanywa huku kwa tani 516,041 za taka inaonesha jinsi Braza linavyowajibika katika kuhakikisha Sheria ya Mazingira inayozingatia uhifadhi na utunzaji wake unazingatiwa na ndio maana pia tumetoa jumla ya vibali 174 vya kushughulika na taka hatarishi ndani ya Nchi yetu.” amesema Dkt. Gwamaka.

uharibifu wa Mazingira kwa kuchoma Misitu.

Hata hivyo  amebainisha kuwa usimamizi wa tafiti za Mazingira huku ikifanikiwa kuratibu uteuzi wa Eneo la Rufiji-Mafia-Kibiti-Kilwa (RUMAKI), ikiwa na lengo la kujumuishwa katika mtandao wa kidunia wa Hifadhi za Binadamu na Hifadhi hai.

Lishe Shuleni: Chalamila awaita Wazazi, Maafisa Elimu
Mshindi wa Nobel afungwa miaka 10 jela