Mahakama nchini Belarus imemhukumu kifungo cha miaka kumi jela, mwanaharakati Ales Bialiatski aliyeshinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2022.

Bialiatski pamoja na viongozi wengine watatu wa taasisi ya kupigania haki za binadamu ya Viasna Human Rights Centre wamehukumiwa leo baada ya kukutwa na hatia ya kufadhili maandamano na kuingiza fedha nchini humo kinyume cha utaratibu.

Kiongozi wa upinzani, Sviatlana Tsikhanouskaya amesema kifungo walichopewa hakikuwa cha haki na kwamba watafanya mpango wa kukata rufaa.

“Tunapaswa kufanya kila liwezekalo kupinga hatua hii ya kutowatendea haki na kwamba waachiwe,” ameandika Twitter.

Awali, waendesha mashtaka waliiomba Mahakama kuwafunga kifungo cha miaka cha miaka 12 jela.

Shirika la habari la Taifa la Belarus limethibitisha kifungo hicho.

Malalamiko 369 uharibifu wa Mazingira yatua NEMC
Fatma Karume: Feisal Salum analazimishwa