Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Watanzania hasa wale wanaoishi pembezoni mwa mradi wa Ujenzi wa Umeme katika Bwawa la Mwalimu Nyerere – JNHPP, wanatarajia kunufaika na matumizi ya rasilimali hiyo katika kujiletea maendeleo.

Makamba ameyasema hayo hii leo Aprili 25, 2023 katika eneo la ujenzi wa mradi huo unaofanyika katika mto rufiji, na kuongeza kuwa mbali na lengo la upatikanaji wa nishati pia Wqnanchi hao wataweza kufanya shughuli za Kilimo na uvuvi.

Waziri wa Nishati, Januari Makamba akizungumza na Mwandishi wa Habari kuhusu Mradi wa JNHPP.

Amesema, “huu mradi ni wa wananchi wote na jamii jirani ni lazima itanufaika mfano mto Nile watu wanaendesha shughuli zao za kiuchumi pale lakini kuna miradi ya kitaifa inayoendelea na hata hapa kwetu lazima watanufaika hauwezi kutenganisha.”

Ujenzi wa mradi wa Bwawa la umeme la JNHPP, umefikia asilimia 85.06, na  Serikali tayari imeainisha maendeleo ya mradi hadi kufikia mwezi Machi 2023 ikiwepo kazi ya uchepushaji Mto (Diversion Works), iliyofikia asilimia 99.63.

Serikali yaridhishwa kasi ujenzi mradi wa umeme JNHPP
Rais Mwinyi asifu miaka 59 ya Muungano