Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na msemaji wa NIDA, Geophrey Tengeneza ametaja sababu za kitambulisho cha taifa kuchelewa kutoka, ikitokana na mambo ya kiusalama,) kwani kitambulisho hicho ni tofauti na vingine.

Tengeneza ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media na kueleza kuwa kitambulisho hicho kimebeba taarifa nyeti na za muhimu za mwananchi na kinatumika mahali popote pa huduma ambazo zitahitaji NIDA.

“kitambulisho ambachohiki ni lazima tuhakikishe kwa kina,usahihi na kina kwenda kwa mtu ambaye ni sahihi kwa misingi iyo kina taratibu zake na ni tofauti na vitambulisho vingine”.

Tengeneza ameongeza kuwa, “pia taratibu za kujiridhisha kwamba kweli huyu ndiye na si mtu mwingine na tunatoa kitambulisho kwa mtu ambaye ni sahihi na ni mtanzani na si mtu wa njee.”

“Vinginevyo tukienda kwa haraka haraka inaangukia kutoa kitambulisho kwa mtu ambaye si mtanzania na pengine sio mtu anayestahili kwahiyo inaweza kuhatarisha usalama wan chi na hata usalama wa watu,” amesema.

Msemaji huyo wa NIDA amesema kuwa mchakato wa kujirishisha katika kutoa utambulisho na kitambulisho cha taifa haufanywi na NIDA pekee unafanywa na wadau wengine wakiwemo TAMISEMI na UHAMIAJI.

Amesema, “lakini pia idara ya uhamiaji na wao wana sehemu ya kujiridhisha kama ilivyo kwa TAMISEMI wewe ni raia wa Tanzania kweli hakuna tatizo lolote si mtu wa kutoka njee wakishajiridhisha ndipo mchakato unaendelea mpaka hatua ya mwisho ya kupata kitambulisho.”

TASAF iwakwamue walengwa - Simbachawene
Rais Samia aagiza mageuzi haki jinai