Kiungo kutoka nchini Ujerumani Bastian Schweinsteiger, huenda akaanza katika kikosi cha kwanza cha Man utd katika mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) ambaop utawakutanisha na West Ham Utd katika uwanja wa Old Trafford.

Kiungo huyo hajawahi kuanzishwa katika klikosi cha kwanza tangu meneja Jose Mourinho alipotua klabuni hapo mwezi Julai mwaka huu, na aliwahi kuambiwa hana nafasi klabuni hapo.

Kiungo huyo ambaye alicheza michezo 121 na kufunga mabao 24 akiwa na timu ya taifa lake la Ujerumani, ameonyesha uvumilivu na wakati mwingine hutakiwa kufanya mazoezi la kikosi cha wachezaji wa akiba.

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England umebaini kuwa, Mourinho amejipanga kumtumia Schweinsteiger katika mchezo wa hii leo, kufuatia pigo linalomkabili la kumkosa Paul Pogba anaekabiliwa na adhabu ya kuonyeshwa kadi tano za njano.

Kuna uwezekano mkubwa kwa Schweinsteiger kuondoka mwishoni mwa msimu huu, lakini bado haijaelezwa ni wapi atakapolekekea kwa lengo la kumalizia soka lake.

Juventus Yajishtukia Kwa Paulo Dybala
Casimiro Kuanza Kuivutia Kasi El Clasico