Klabu ya Man Utd italazimika kujibu mashtaka mbele ya chama cha soka nchini England (FA), kwa kosa la kushindwa kuwatuliza wachezaji wao wakati wa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Chelsea uliochezwa usiku wa kuamkia jana jijini London.
FA imefungua mashtaka dhidi ya klabu hiyo ya Old Trafford, baada ya kujiridhisha kulikua na ulazima kwa viongozi wa benchi la ufundi la Man Utd kuwatuliza wachezaji wao wakati wote wa mchezo, lakini hali hiyo ilishindikana na kusababisha vitendo vya utovu wa nidhamu.
Katika mchezo huo, wachezaji wa Man Utd walionyesha kuwa na hasira na visasi dhidi ya wapinzani wao, ambao walimaliza dakika 90 wakiwa mbele kwa bao moja, lililofungwa na kiungo kutoka Ufaransa N’Golo Kante.
Man utd wamepewa muda hadi Machi 17 (siku ya ijumaa) kukubali ama kakataa mashtaka hayo.