Rapa wa Nako 2 Nako, Lord Eyez amewapa neno vijana na mashabiki wake kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, akiwataka kukaa nayo mbali.

Akifunguka kupitia E-TV, Eyez ameeleza kuwa dawa za kulevya hazijaribiwi kwani ukigusa unazama na kutoka sio rahisi.

“Dawa za kulevya zimekuwa shida hasa kwa vijana, wengi wanateketea. Mimi nataka niwaambie kuwa dawa za kulevya hazijaribiwi,” alisema.

“Usiguse, usinuse, usitumie dawa za kulevya kwa sababu ni hatari. Zitakuangamiza,” aliongeza kiongozi huyo wa N2N.

Katika hatua nyingine, Lord Eyez ambaye amekuwa akikanusha vikali kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya, amewataka mashabiki kujipanga kupokea ngoma nyingi zaidi kutoka kwake.

“Hii ‘Hela yangu Ntaipataje’ ni kama nimewatekenya tu ili tucheke wote, halafu niachie ngoma nyingine mfululizo,” alifunguka.

Alisema kuwa kuna nyimbo nyingi amefanya kolabo za wasanii kadhaa ikiwa ni pamoja na Barakah Da Prince anayesimamia kazi zake pamoja na G-Nako.

Rais wa CAF akataa kupokea mshahara
TFF yatoa salamu za rambirambi shule ya Lucky Vincent