Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza ng’ombe waliobaki hai kati ya 692 waliokufa katika Pori la Akiba la Rukwa/Lwafi, waliokuwa wameshikiliwa warudishwe kwa wamiliki wa mifugo hiyo.

Akiwa katika ziara yake, Mpina ametoa maamuzi hayo baada ya kukuta mizoga 692 ya ng’ombe ikiwa imetapakaa katika Pori hilo ambapo imedaiwa kuwa ng’ombe hao walikufa kwa kukosa marisho.

Aidha, imeelezwa kuwa mazingira hayo yamechangia kasi kubwa ya maambukizi ya magonjwa nyemelezi kuwa kubwa zaidi na kupelekea ongezeko la vifo kwa mifugo hiyo ambayo ilikuwa katika pori hilo.

Hata hivyo baada ya kushudia Mizoga hiyo, Mpina amepokea taarifa ya Mkoa, Wahifadhi, Chama cha Wafugaji na wamiliki wa mifugo hiyo na kupitia nyaraka mbalimbali, ilibainika kuwa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, ilitoa amri ya ng’ombe hao kukabidhiwa kwa wenyewe tangu Julai 27, mwaka jana.

Video: Siri ya kikao cha Nyalandu na Lowassa Dar, Deni la Taifa lapanda
Nyaraka za Zitto Kabwe zachunguzwa