Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa viongozi wote waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.

“Ninafahamu kuwa kuna ugawaji wa vitalu kinyume na sheria ambao nimeusitisha na nitafuatilia vitalu alivyogawa mtangulizi wangu Nyalandu kinyume na sheria na mkurugenzi aliyekuwepo nitawachukulia hatua,” amesema Kigwangalla

Aidha, amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.

 

Miaka miwili ya JPM yaimarisha huduma Muhimbili
Serikali kutenga trilioni 7.6 kulipa mishahara