Takriban watu wawili wameuawa jijini Nairobi wakati maafisa wa polisi wakikabilina na wafuasi wa kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, huku gari moja la polisi likichomwa moto.
Umati mkubwa wa watu ulikuwa umekusanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,kwaajili ya kumpokea kiongozi huyo aliyekuwa anarejea kutoka ziarani Ulaya.
Aidha, mabomu ya machozi yalirushwa sehemu mbalimbali katika mikusanyiko ya wafuasi hao kwaajili ya kuwatawanya lakini wafuasi hao walianza kujibu mashambulizi hayo kwa kuwarushia mawe askari polisi.
Hata hivyo, Siku ya Jumatatau Mahakama ya juu nchini Kenya inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uhalali wa uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba ambao rais Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.