Kocha mkuu wa Kagera Sugar, Adolph Richard amesema hali ya kikosi chake si mbaya licha ya kutetereka kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.

Richard ameelezea matumaini yake huku kikosi chake kikitarajia kupambana na Majimaji FC hii leo na kujinadi kuwa kila mchezo kwao ni fainali na huenda wakaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Bado halijazama (jahazi la timu yake), kila mchezo kwetu ni fainali, Inshaallah mambo yakienda sawa tunaweza kuibuka na ushindi” alisema Adolph Richard baada ya kuulizwa kuhusu mwenendo wa timu yake.

Mohammed Adolph Richard

Kagera Sugar haipo kwenye nafasi nzuri kwenye msimu huu, sababu kubwa inayotajwa kuifanya timu hiyo isifanye vizuri ni kuondoka kwa baadhi ya nyota wake kama Themi Felix, Atupele Green na Rashid Mandawa ambao wamekosa mbadala wao.

Sababu nyingine ni kukosa faida ya uwanja wa nyumbani baada ya uwanja wao wa Kaitaba kuwa katika matengenezo ya kuwekewa nyasi bandia.

Samatta: Watanzania Wanaweza Kucheza Ulaya
Mengine Yaibuliwa Kuhusu Uhamisho Wa Neymar