Mtandao huu ulitaka kujua jinsi gani kuna utofauti katika maisha ya Mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta ambaye anakipiga nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk, ukilinganisha na alivyokua Tp Mazembe ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kupitia njia ya mtandao wa kijamii wa Facebook, Samatta aliwasiliana na mwandishi wa taarifa hizi na kuanika ukweli wa maisha yake ya nchini Ubelgiji tangu alipotambulishwa rasmi mwishoni mwa juma lililopita, kama mchezaji rasmi wa KRC Genk.

 

“Maisha ni tofauti kwa vitu vingi vyakula, baridi Maisha hayawezi kufanana wanaocheza soka Tanzania, wengi wana vipaji wanaitaji kuja kucheza Ulaya wanaweza” Alijibu Samatta katika ukurasa wake wa Facebook

 

Utata: Ndege yapata ‘tobo’ kubwa angani
Adolph Richard Awakingia Kifua Kagera Sugar