Katika hali iliyoacha maswali mengi, ndege kubwa iliyokuwa imebeba abiria 60 imelazimika kutua ghafla mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya kupata tobo kubwa ikiwa angani.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Daallo iliyokuwa ikirejea Djibouti ilikuwa imeruka umbali wa mita 3,048 angani ilibainika kuwa na shimo kubwa ubavuni.

Ingawa bado shirika hilo na Mamlaka za Somalia hazijaeleza chanzo cha tobo hilo, baadhi ya ripoti zimeeleza kuwa ndege hiyo ilishika moto muda mfupi baada ya kupaa.

Maafisa wa Polisi waliwaambia waandishi wa habari kuwa watu wawili walipata majeraha kufutia tukio hilo.

“Hakukutokea mlipuko, ni kiunzi cha ndege kilichopata hitilafu wakati ndege ilipokuwa futi 10,000,” Dareen Howe, rafiki wa abiria mmoja aliyekuwa amepanda ndege hiyo aliiambia BBC.

 

Mwalimu aishi darasani miaka 10 kushinikiza alipwe stahiki zake
Samatta: Watanzania Wanaweza Kucheza Ulaya