Afrika ndilo Bara lenye Vijana wengi zaidi, ambapo takwimu zinaonesha kuwa ifikapo mwaka 2050, Africa itatoa Nchi 10 zenye idadi kubwa zaidi ya vijana Duniani, huku zaidi ya asilimia 60 wakiwa ni Vijana walio chini ya umri wa miaka 25.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo hii leo Julai 26, 2023 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu Jijini Dar es salaam na kudai inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2023 Africa itakuwa na asilimia 42 ya vijana wote Duniani.
“Hii inatuonesha kuna mambo mengi ya maendeleo tunapaswa kufanya hususani kwenye eneo la afya ili tuweze kukuza wastani wa umri kwa Africa hii ina maanisha bara letu lina watoto na vijana wengi, habari hii ni nzuri na vile vile ni mbaya kwetu itakuwa nzuri na yenye tija iwapo tutawekeza kwenye rasilimali watu kwa kuhakikisha uwepo wa afya bora na elimu bora yenye stadi za maisha,” amesema Dkt. Samia.
Aidha, ameongeza kuwa, ili kujenga nguvu kazi yenye tiga kama ilivyo kwa wenzetu wa bara la Asia tusipofanya hivyo tutaongeza vijana wasio na ujuzi, wasioajirika na vijana wa kujiingiza kwenye vitendo viovu vya kihalifu na uvunjivu wa amani.
Amesema, “sisi tuliopo hapa leo tujiulize je Bara tuliloridhi kwa waasisi wetu waliotafuta uhuru wa Africa ndilo bara tunalotaka kuwaridhisha vizazi vijavyo au wajukuu wetu? Je Africa tunayoijenga leo ni yenye uchumi endelevu au uchumi unaiodumaa tukipata majibu ya hayo, tutalijenga bara letu vema zaidi.”