Bara la Afrika limepata mgao wa dola za kimarekani Bilioni 1.9 kutoka kwa nchi za Muungano wa Ulaya kwa lengo la kupunguza idadi ya wahamiaji wanaofanya safari hatari kuelekea Ulaya.

Viongozi wa Muungano wa Ulaya na Afrika wamesaini makubalino maalum baada ya kuidhinishwa kwa kiasi hicho cha fedha katika mkutano uliofanyika Malta.

Mpango huo unakuja wakati ambapo nchi hizo za Ulaya zinakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 3 wanaweza kufika Ulaya kutafuta hifadhi na nafasi za kazi hadi kufikia mwaka 2017.

Tanzania ni moja kati ya nchi zitakazofaidika na hazina hiyo iliyotengwa. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Djibouti, Somalia, Sudan Kusini, Ethiopia pamoja na Eritrea.

Lowassa Kutoa Ya Moyoni Jumamosi Hii
NEC Yaingilia Kati Ushawishi Kwa Rais Kuhusu Baraza La Mawaziri