Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva amewataka wanaharakati kumpa nafasi Rais John Magufuli kufanya maamuzi ya uteuzi wa Mawaziri.

Jaji Lubuva ameyasema hayo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi kumtaka Rais Magufuli kuzingatia usawa wa Kijinsia katika uteuzi wa Baraza lake la Mawaziri.

“Nimesoma gazeti nikaona TGNP wakimshauri Rais Magufuli kuzingatia usawa wa kijinsia kwenye baraza lake la mawaziri. Hiyo naona haikuwa sawa,” alisema Mwenyekiti huyo wa NEC.

“Rais atafanya hivyo baada ya Mamlaka nyingine kukamilisha taratibu zao,” aliongeza.

Alieleza kuwa Rais atafanya maamuzi yake kwa kuzingatia taratibu na kushirikiana na washauri pamoja na wasaidizi wake kama Katiba inavyoelekeza.

Afrika Yapata $1.9 Bilioni Kuzuia Wanaokimbilia Ulaya, Tanzania Yaguswa
"TSHABALALA" Mchezaji Bora Mwezi Oktoba