Mwanamke mmoja amefukuzwa kazi na kampuni aliyokuwa akiifanyia kazi mara baada ya kuuonyeshea kidole cha kati msafara wa Rais wa Marekani, Donald Trump.
Picha hiyo ilisambazwa baada ya kupigwa terehe 28 mwezi Oktoba mjini Virginia karibu na uwanja wa kucheza Gofu wa Donald Trump ambapo alikuwa akiendesha baiskeli hivyo baada ya kukutana na msafara huo alionyesha kidole cha kati.
Juli Briskman amesema kuwa kampuni ya LLC ilimuita katika mkutano siku moja baada ya kumwambia afisa mkuu wa ajira kwamba ni yeye ndiye aliyepiga picha hiyo hivyo ameenda kinyume na utaratibu wa sheria za kampuni.
Hata hivyo, Briskman amesema kuwa aliisisitizia uongozi wa kampuni hiyo kuwa haikuwa ni muda wa kazi wakati alipokuwa akifanya tukio hilo kwani kumfukuza kazi ni kwenda kinyume na haki za mfanyakazi.
-
Mke wa Mugabe ataka makamu wa Rais afutwe kazi
-
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii watakiwa kuongeza bidii
-
Majaliwa ataka ujenzi wa shule ufanyike haraka