Video Vixen maarufu, Agnes Masongange ameendelea kusisitiza kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na star wa Nigeria, Tekno Miles licha ya nyota huyo kumkana kupitia vyombo vya habari.

Baada ya Tekno kusikika kupitia Clouds Fm akieleza kuwa aliwakuwa rafiki wa kawaida wa Masogange na hawajawahi kuvuka mstari wa urafiki wao na kula tunda, mrembo huyo amedai kuwa kuna kitu kinamuumiza Tekno ndio maana anajitahidi kukataa ukweli.

“Niko busy Na maisha yangu cna muda wa drama so plz hizo drama zenu hukohuko na why asiongee yote hayo b4 anajua kitu gani kilichomuuma that’s why anajishtukia ryt now niko next level,” aliandika Masongange Instagram akimjibu shabiki mmoja aliyehoji mkanganyiko wa kauli za wawili hao.

tekno-maso

Hata hivyo, Masongange hakutaka kushindwa kirahisi (japo haijulikani kwanini anataka ifahamike kuwa walikuwa wapenzi), alipost picha zinazomuonesha akiwa na Tekno studioni kwake alipoenda kumtembelea Nigeria na kuongeza picha nyingine inayoonesha kuwa alikuwa amelala kwenye kitanda cha Tekno kwa kufanisha picha hiyo na sehemu aliyojilaza mkali huyo.

tekno-maso-2

Lionel Messi Awakana Mashabiki Maandazi
Hatimaye Mahakama Yatoa Hukumu Kesi Ya 'Mita 200', Iko Hapa