Wakati Young Africans ikijinasibu kuwa tayari kupambana na kuwafunga Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ameibuka na kuwapiga kijembe.

Young Africans itakua mwenyeji wa Al Hilal kesho Jumamosi (Oktoba 08) katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukitarajiwa kuunguruma mjini Khartoum-Sudan mwishoni mwa juma lijalo.

Ahmed Ally amerusha kijembe kwa watani zao wa Jadi akitumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, kwa kuandika ujumbe ambao anaamini Simba SC imekua kichocheo cha kuitamanisha klabu hiyo ya Jangwani kutamani kuifunga Al Hilal kesho Jumamosi.

Ahmed Ally ameandika: Mafanikio ya Simba kwenye michuano ya kimataifa yameamsha waliolala
Leo hii unawaona Utopolo wana hangaika kutaka kuwafunga Al Hilal kwa sababu Simba tumeshafanya hivyo na wao wanatamani sasa.

Miaka mitano nyuma wasingehangaika na wangejua safari yao imeishia hapo.

Sisi tumewaamsha, tumewaonesha dira, hawajahi kuwa na hamu ya kimataifa lakini safari hii wanayo ni kwa sababu ya Simba.

Na wao wanataka kuwa kama Simba, sisi ndo role model wao, hawasemi kwa sauti lakini wakikaa peke yao wanasema tunatamani kuwa kama Simba.

Kituo magonjwa ya mlipuko kujengwa Kagera
Bigirimana awaita mashabiki Kwa Mkapa