Kiungo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Gael Bigirimana amewataka Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kufika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wingi kesho Jumamosi (Oktoba 08).

Young Africans itakua mwenyeji wa Al Hilal kesho Jumamosi (Oktoba 08) katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukitarajiwa kuunguruma mjini Khartoum-Sudan mwishoni mwa juma lijalo.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Ijumaa (Oktoba 07), Kiungo huyo kutoka nchini Burundi amesema, wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo dhidi ya Al Hilal, lakini nguvu kubwa ya kupambana wanaihitaji kutoka kwa Mashabiki na Wanachama ambao watajitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kesho.

Amesema Wachezaji wote wa Young Africans wanatambua umuhimu wa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kuhakikisha wanashinda, ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kabla ya kwenda Khartoum-Sudan juma lijalo kwa mchezo wa Mkondo wa Pili.

“Kama wachezaji tunajua umuhimu wa mechi hii na wachezaji wote wameshajua ni namna gani ilivyokuwa ngumu kwenda kushinda mechi hii ugenini hivyo kila mmoja anafahamu kuwa mechi hii itachezwaje.”

“Young Africans ina wachezaji wapya itakuwa mara yangu ya kwanza kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa namna tunavyofahamu matarajio ya mchezo, tunajua tunatakiwa kujituma na nina furaha kuwa mmoja kati ya kikosi kitakachocheza kesho.”

“Tunahamasishana sisi wenyewe ili kutengeneza morali baina yetu kwa ajili ya mchezo huo mchezo huo, hivyo ninawasisitiza Mashabiki wafike kwa wingi Uwanjani kesho ili kutupa morari zaidi ya kupambana na kufikia lengo la kupata ushindi nyumbani.”

“Nimeshacheza Ligi Kubwa Ulaya, Shabiki ana sifaa kubwa ya kuwafanya wachezaji kupambana na kujihisi wana deni kubwa la kurejesha fadhila ya ushindi, kufika kwenu Uwanjani kutasaidia sana kwa wachezaji kujituma bila kuchoka.” amesema Bigirimana

Young Africans ilitinga Mzunguuko wa Kwanza kwa matokeo ya jumla 9-0 dhidi ya Mabingwa wa Sudan Kusini Zalan FC, huku Al Hilal ikisonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, kufutia ushindi wa jumla wa sare ya 2-2.

Ikicheza ugenini Ethiopia dhidi ya St George mwezi Septemba Al Hilal ilikubali kufungwa 2-1, kabla ya kuibuka na ushindi wa 1-0 mjini Khartom.

Ahmed Ally aichana Young Africans
GGML yadhamini Mkutano Mkuu ukuzaji fani Jiolojia