Meneja wa Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally amekiri kupokea taarifa za kukosolewa kwa kikosi chao, baada ya mchezo wa jana Jumanne (Machi 07), dhidi ya Vipers SC ya Uganda.

Simba SC ilicheza mchezo wa Mzunguuko wanne wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika katika Uwanja wa nyumbani Benjamin Mkapa na kupata ushindi wapili mfululizo dhidi ya Vipers SC.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii kukubali changamoto zinazozungumzwa na Waandishi wa Habari pamoja na Wachambuzi kupitia vyombo vya habari, lakini bado akasimamia sababu ya ushindi ambayo imewaongezea alama na kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya Raja Casablanca ya Morocco.

Ahmed Ally ameandika: “Ukisikiliza Radio unaweza kujua Simba ndo imefungwa jana, halafu ukisiliza tena unaweza kudhani Simba ndo ina point moja kwenye kundi letu, halafu ukitega sikio vizuri unaweza kuhisi kwamba Simba hakuna kitu kizuri tumefanya jana ?

Ila sisi ndo tunapenda mtukosoe hadi tufike Nusu Fainali tuliyokusudia.”

Ushindi wa 1-0 dhidi ya Vipers SC umeiwezesha Simba SC kufikisha alama 06 katika msimamo wa Kundi C, ikitanguliwa na Raja Casablanca yenye alama 12, huku Horoya AC ya Guinea ikiendelea kubaki na alama 04.

Vipers SC inayoshiriki Michuano hiyo Hatua ya Makundi kwa mara ya kwanza inaburuza mkia wa Kundi C kwa kuendelea kuwa na alama moja, huku ikipoteza michezo mitatu.

Historia imeandikwa: Rais Samia ndani ya Kongamano BAWACHA
Serikali yakemea wizi wa mazao na mifugo mwezi mtukufu