Takriban Watu sita wamefariki dunia na wengine 49 kujeruhiwa kufuatia kutokea kwa ajali iliyohusisha Lori na Basi la abiria katika eneo la Chigongwe llililopo jijini Dodoma.

Ajalinhiyo, imetokea Machi 4, 2025 majira ya saa 4 usiku ambapo Lori hilo ni lile lenye namba za usajili T405 BYS, na Basi la AN Classi lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Kigoma.

Lori hilo lilikuwa limeharibika barabarani bila ya kuweka alama za tahadhari  huku mashuhuda wakisema pia mwendokasi wa basi huenda ulichangia ajali hiyo.

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amesema majeruhi wanatibiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Miili ya marehemu inasubiri utambuzi wa ndugu.

Wizara ya Nishati inajivunia kuwawezesha Wanawake kiuchumi - Kapinga