Watu watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Nyambari, Lari kaunti ya Kiambu nchini Kenya leo Julai 9, 2021 iliyohusisha lori na matatu mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 14 kila moja.

Aidha Majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kijabe na kupatiwa matibabu, ambapo wamedaiwa kuwa wapo katika hali mahututi, Kati ya walipoteza maisha, watatu ni wanaume na wawili ni wanawake.

“Nimewasiliana na usimamizi wa hospitali ya Kijabe na imethibitishwa kwamba watu 5 walipoteza maisha yao na sita kujeruhiwa vibaya kwenye ajali hiyo,” Amesema Kirui.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda Mkuu wa Polisi Stephen Kirui amesema idara ya trafiki imeanza kufanya uchunguzi ili kubaini nini chanzo cha ajali hiyo.

Aidha Kamanda Kirui amewahasa madereva wote kuwa makini na waangalifu, kwani hali ya anga sio nzuri katika maeneo hayo, huku akisema hataki kuripoti maafa zaidi kutokana na ajali,” aliongezea Kirui.

Wanne wasajiliwa 'MASANDAWANA'
Tanzania kushirikiana na UNEP utunzaji mazingira