Klabu ya Mamelodi Sundown imetangaza Usajili wa wachezaji wanne ambao wamejiunga na Wabrazil kwa mikataba ya miaka mitano kuanza na msimu mpya wa 2021/22.

Wachezaji hao Ni Pamoja Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Slovakia Pavol Šafranko ambaye amejiunga na Masandawana kutoka Romania katika klabu ya Sepsi OSK SF. Šafranko alifunga mabao tisa na kutoa pasi sita za magoli katika Michezo 33.

Beki wa kushoto wa kimataifa wa Zimbabwe Divine Lunga kutoka Golden Arrows. Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye alicheza mechi ishirini na sita za ligi msimu uliopita, anajiunga na Wabrazil kwa mkataba wa muda mrefu. Lunga hivi karibuni alijumuishwa kwenye kikosi cha awali cha Zimbabwe kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia zijazo.

Kiungo mshambuliaji Neo Maema anajiunga na Wabrazil kutoka Bloemfontein Celtic baada ya mkataba wake kumalizika Maema alicheza mara 17 kwenye ligi ya ndani akifunga mabao 3 katika msimu uliopita.

Downs pia wamepata huduma ya Grant Kekana kutoka SuperSport United FC. Beki huyo mwenye umri wa miaka 28 alicheza mechi 19 msimu uliopita

Wachezaji Polisi Tanzania wafanyiwa uchunguzi KCMC
Ajali iliyohusisha magari 3 yaua 5