Takribani Watu 20 hawajulikani walipo baada ya kiboko kugonga boti waliyokuwa wakisafiria na kupelekea kupoteza mwelekeo na kuzama kwenye Mto Shire uliopo eneo la Nsanje kusini mwa nchi ya Malawi.
Kwa mujibu ofisa wa ngazi ya juu wa eneo la Nsanje, Robert Nayeja amesema boti hiyo ilikuwa na watu 37 waliokuwa wakielekea mashambani kwa ajili ya shuguli zao za kila siku eneo la upande wa wa nchi ya Msumbiji.
Aidha, Nayeja amesema katika tukio hilo na juhudi za uokoaji mwili wa mtoto mchanga uliopolewa akiwa ni miongoni mwa mtoto wa wazazi waliokuwa wakisafiri waliokuwa kwenye boti hiyo.
Hadi sasa watu 13 wameokolewa wakati huu na maofisa wa polisi wanasema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka wakati ambapo vitengo vya uokozi vikiendelea kuwatafuta watu waliozama.