Wananchi jamii ya Wafugaji nchini Kenya, wakiwa na hasira kali wamewauwa Simba wanne kutokana na Wanyama hao wakali kushambulia mifugo yao huku Serikali ikielezea wasiwasi wake kufuatia simba wengine sitakuuawa wiki jana na kufanya idadi kuwa 10.

Kati ya Simba hao waliouawa, yupo dume aitwaye Loonkiito (19), aliyelitajwa kuwa dhaifu na Shirika la Huduma ya Wanyamapori la Kenya, ambalo lilisema alitoka nje ya mbuga ya kitaifa ya Amboseli hadi kijijini, kutafuta chakula.

Simba wengine sita kutoka katika mbuga hiyo ya kitaifa waliuawa kwa kupigwa mikuki na wafugaji baada ya mifugo yao (mbuzi 11) kuliwa na Simba hao katika eneo la Mbirikani, kaunti ya Kajiado na kusababisha mvurugano kati ya binadamu na wanyamapori ambao umeitia wasiwasi serikali.

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika katika Jumuiya ya Kimataifa ya Kulinda Wanyama, Tennyson Williams alisema upotevu wa makazi na mabadiliko ya hali ya hewa unatishia idadi ya simba porini na kwamba mustakabali wao unaonekana kuwa mbaya.

“Wanyamapori ni mali ya porini na hivyo tuwaruhusu wawepo porini. Tunapaswa kuwa na vifungu vya kisera vilivyo wazi kabisa vinavyotekelezeka ambavyo haviruhusu ubinadamu kuvamia na kumaliza rasilimali zinazopaswa kuwawezesha wanyama hawa kujiendeleza,” alisema.

Serikali na vikundi vya uhifadhi vina mpango wa kutoa fidia kwa wafugaji ambao mifugo yao inauawa na wanyama pori lakini hata hivyo, wafugaji wamekuwa wakijilinda zaidi baada ya kupoteza mifugo kutokana na ukame ambao umetajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa huko ukanda wa Afrika Mashariki.

Wafanyabiashara wakubaliana na Waziri Mkuu
Chalamila aacha wosia Karagwe, akina mama watabasamu