Jumla ya watu 12 wamefariki kufuatia ajali ya lori la mafuta ya petroli kuanguka kwenye barabara kuu na kisha kulipuka katika Jimbo la Kogi kaskazini mwa nchi ya Nigeria.
Msemaji wa Polisi Kogi, William Ovye amesema Lori hilo, lilipata ajali baada ya kutokea kwa hitilafu ya breki kando ya barabara kuu eneo la Halmashauri ya Ofu usiku wa Alhamisi Novemba 10, 2022 na kisha kugongana na gari na kusababisha kuruka kwa moto.
Amesema, “Gari hili liliponda magari yaliyokuwa yamepaki njiani na watu 12 waliuawa yaani wote waliteketezwa hadi kufa, alisema Aya pamoja na amri ya polisi ya Kogi.
Shuhuda wa tukio hilo, Bisi Kazeem akiwa na Kikosi cha Shirikisho la Usalama Barabarani cha Nigeria alisema watu 18 walihusika katika ajali hiyo huku saba wakipata “majeraha mbalimbali na wengine 11 waliosalia wakiteketea kiasi cha kutotambulika.
Ajali kama hizo ni za kawaida kando ya barabara kuu nchini Nigeria, huku hatua mpya za askari wa usalama barabarani zikishindwa kuzuia ajali na kufanya Kogi kujulikana kuwa ni eneo la moto na zaidi ya watu 10 waliuawa katika ajali sawa na ile ya Septemba 2022.