Takriban watu 22 wamefariki dunia katika ajali ya boti ya utalii iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya 30 kusini mwa nchi ya India.
Afisa wa Polisi, Abdul Nazar amesema makundi ya waokoaji yanatarajia kupata miili zaidi kutoka ndani ya boti hiyo, baada ya kuikokota kutoka kwenye mlango wa Mto Poorappuzha, karibu na mji wa Tanur.
Waziri wa michezo wa India Vii Abdurahiman amesema miongoni mwa wahanga wamo watoto waliokuwa katika matembezi baada ya kumaliza muhula wa shule.
Wakati huo huo, watu wawili wameuawa katika jimbo la Rajasthan huko huko India, baada ya ndege ya kijeshi chapa MiG-21 kuanguka katika nyumba yao ambapo Jeshi la anga la India limesema rubani wa ndege hiyo alinusurika.