Takriban watu 10 wamefariki na wengine 10 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa ajali ya Lori lililowagonga watembea kwa miguu na waendesha Bodaboda katika eneo la Migori lililo karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Migori, Mark Wanjala amesema ajali hiyo ilitokea kando ya barabara kuu wakati dereva aliposhindwa kudhibiti breki ambapo juhudi za kuwaokoa watu waliokuwa wamenaswa chini ya Lori, ilikuwa ikiendelea.

Amesema, watu wengine wawili kati ya hao 10 pia walifariki baada ya kuripotiwa kuangushwa kwenye daraja na kuingia mtoni na jaribio la kuwaokoa halikuweza kuzaa matunda huku mashuhuda wakisema Lori hilo lilikuwa likipiga honi mara kwa mara kabla ya ajali hiyo.

Aidha, wamesema Lori hilo lilikuwa limebeba magunia ya mchele kuelekea mji wa mpaka wa Isebania hadi nchi jirani ya Tanzania na picha za Video za watu wakipora mchele bila kuwasaidia waliokuwa wamenaswa chini ya Roli tayari zimesambaa katika mitandao ya kijamii.

China yazindua mazoezi ya kijeshi kuikabili Taiwan
Wachezaji Simba SC wapigwa marufuku