Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika dua ya kuwaombea marehemu waliofariki dunia katika ajali ya ndege, itakayofanyika Novemba hii leo Novemba 7, 2022 katika Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ambaye amesema sambamba na taarifa hiyo manusura wa ajali hiyo pia hali zao zinaendelea vizuri.
Jana, Novemba 6, 2022 Waziri Mkuu Kassim aliwasili Mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.
Waziri Mkuu pia aliwajulia hali wahanga wa ajali hiyo waliokuwa wakipata matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambao walikolewa katika ajali hiyo.