Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma  wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Hellen Semi amefariki katika ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi.

Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kifo cha mkurugenzi huyo. Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea leo asubuhi katika eneo la Chalinze mkoani Pwani.

Mwamwaja ameeleza kuwa, Mkurugenzi wa huduma za kinga wa wizara hiyo, Dk. Neema Rusibamayila alijeruhiwa katika ajali hiyo.

Watumishi hao wa wizara walikuwa safarini wakitoa Dar es Salaam kwenda mjini Dodoma kuhudhuria mkutano wa waganga wa mikoa uliopangwa kuanza kesho.

Babu Seya, Papii wafunguka kuhusu barua inayodaiwa wamemuandikia Rais Magufuli
Trump ataka Clinton afanyiwe vipimo vya matumizi ya dawa kabla ya mdahalo