Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Antony Lugendo (34)mkulima,mkazi wa Mlandizi kwa kosa la kumdhalilisha mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka mitatu kwa kumchezea chezea sehemu za siri.
Aidha mtuhumiwa alikamatwa akiwa chumbani kwake akiwa amemvua nguo zote huku akimchezea mtoto huyo ambae ni mwananfunzi wa chekechea.
Akithibitisha kutokea kwa tukio Hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Wankyo Nyigesa, amesema upelelezi unaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa.
Katika hatua nyingine, Kamanda Wankyo amesema katika kipindi cha wiki mbili kuanzia septemba 3 hadi 17 septemba Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limefanya operesheni katika wilaya zake tano ikiwa na lengo la kuzuia na, kudhibiti uhalifu.
Katika operesheni hiyo wamefanikisha kukamata bunduki 1 aina ya shortgun yenye namba GP 719 na risasi moja ,bangi kwenye beg ,puli 39 ,kete 661 na miche 24,radio 2 aina ya sony na sabufa moja na spika 6 kati ya hizo aina ya boss 2 na aina ya sony nne, mafuta ya dizel lita 230, petrol lita 500 ,pikipiki moja aina ya boxer yenye namba za usajili MC 226 CMT rangi nyeusi na televisheni tano aina ya Good vision ,sony , Samsung,LG na TCL moja.
Vitu vingine ni desktop moja aina ya dell na CPU mbili ,gari aina ya canter moja ,matairi mawili ya gari , camera mbili aina ya Samsung moja ,camera monitor,mkasi wa kukatia chuma ,funguo master key na pombe ya moshi lita 65.
Sambamba na hayo yote Kamanda Wankyo amewahasa wananchi na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya unyanyasaji kwa watoto kwani kwa kufanya hivyo wanaharibika kisaikolojia.