Klabu ya Al Ahly imekiandikia barua Chama Cha Soka nchini Misri (EFA) wakitaka marefa wa kigeni kuchezesha mchezo wa ‘Super Cup’ na michezo ya ligi iliosalia.

Malalamiko hayo yanakuja siku kadhaa baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Tala’a El-Gaish huku mahasimu wao Zamalek wakishinda kwa kuifunga Wadi Degla bao 1-0, matokeo ambayo yamewaweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa nchini Misri.

Zamalek inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 73 wakifuatiwa na Al Ahly mwenye alama 69, huku wote wakibakiza michezo mitatu tu kumaliza msimu.

Zamalek wanahitaji alama 6 tu kwenye michezo hiyo mitatu, ili kutetea ubingwa.

Rais Samia awasili Zanzibar akitokea Nchini Malawi
Wakuu wa Nchi za SADC wahitimisha mkutano kwa kishindo