Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Malawi Joyce Banda Lilongwe nchini Malawi. Rais Mstaafu Joyce Banda alifika Lilongwe kuzungumza na   kumpongeza Rais Samia kwa kuwa Rais wa kwanza Mwanamke nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais Mstaafu wa Malawi Joyce Banda mara baada ya mazungumzo yao yaliofanyika Lilongwe nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiondoka katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu mara baada ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu uliopo Jijini Lilongwe nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwasili Zanzibar wakati akitokea nchini Malawi ambapo alishiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo tarehe 18 Agosti nchini Malawi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati akitokea nchini Malawi leo tarehe 18 Agosti, 2021.
PICHA NA IKULU

Luis Miquissone awaaga Msimbazi
Al Ahly maji ya shingo Misri