Wapiganaji wa Al-shabab nchini Somalia wameteka eneo la Halgan katikati mwa jimbo la Hiranhilo nchini Somalia muda mfupi tu baada ya Ethiopia kuondoa majeshi yake katika maeneo hayo.

Wanajeshi wa Ethiopia wanaopigana na wapiganaji hao wa Jihad nchini Somalia wameondoka katika kambi kubwa ya kijeshi huko Halgan katikatiki mwa jimbo la Hiran hali iliyopelekea mamia ya watu kuanza kulitoroka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kundi hilo.

Taarifa zinaeleza kuwa ni mara ya tatu mwezi huu, wanajeshi wa Ethiopia kuondoka katika kambi muhimu nchini Somalia ambapo imedaiwa kuwa huenda wanajeshi hao watahitajika kukabiliana na maandamano yanayoendelea nchini mwao.

Picha: Maonyesho ya urembo 'Mr na Ms' Albino Kenya
Gambo aagiza Posho sh10,000 tu kwa madiwani Arusha, aweka sharti kuipata