Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Italia Andrea Pirlo ametangaza kustaafu kucheza soka baada ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya New York City.
Pirlo mwenye umri wa miaka 38 amewahi kuvichezea vilabu vya Inter Milan, Ac Milan, Brescia na Juventus kabla ya kujiunga na Ligi Kuu ya Soka Amerika Kaskazini miaka miwili iliyopita huku pia akiichezea timu ya taifa ya Italia mechi 116 na kuwasaidia kushinda Kombe la Dunia mwaka 2006.
Pirlo alihamia New York kabla ya kuanza kwa msimu wa mwaka 2015 akicheza na kiungo wa kati wa zamani wa England Frank Lampard na mshambuliaji wa zamani wa Hispania David Villa chini ya kocha Patrick Viera lakini hakuweza kushinda vikombe akiwa nao.
-
West Ham yamtimua Slaven Bilic
-
Picha: Taifa Stars yaanza mazoezi ya kuikabili Benin
-
Said Ndemla kuondoka kesho
Tangu aanze kucheza soka Pirlo amebeba kombe la Italia Serie A mara 6, kombe la Copa Italia mara 2, kombe la champions league mara 2 na kombe la dunia mara 1 katika jumla ya michezo 872 aliyocheza.