Klabu ya West Ham imemfuta kazi kocha Slaven Bilic kufuatia mwenendo mbaya wa klabu hiyo katika ligi kuu ya Uingereza.

West Ham ipo katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa EPL na ameshinda michezo miwili tu ya ligi kuu katika michezo 11 iliyocheza msimu huu huku ikipoteza michezo 6 na kusuluhu michezo mitatu.

Makocha wasaidizi Nikola Jurcevic, Edin Terzic, Julian Dicks pamoja na Miljenko Rak nao wameondoka katika klabu hiyo huku kukiwa na taarifa za kocha wa zamani wa Everton na Man Utd David Moyes kuchukua mikoba ya Bilic.

Kama Moyes atateuliwa kuwa kocha wa West Ham ataiongoza kwa mara ya kwanza katika mchezo walgi kuu dhidi ya Watford utakaopigwa tarehe 19 mwezi huu katika uwanja wa Vicarage Road.

Bilic alijiunga na West Ham mwaka 2015 na aliiongoza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya saba ikiwa na pointi 62 na kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu ambao ulikuwa wa mafanikio kwa kocha huyo.

 

 

JPM kufanya ziara nchini Uganda
LIVE: Rais Magufuli katika akizinduzi uwanja wa ndege Kagera