Washika bunduki wa Ashburton Grove (Arsenal) wamaingia katika vita kali na klabu ya Everton ya kumuwania mshambuliaji kutoka nchini Ukraine na klabu ya Dynamo Kiev, Andriy Yarmolenko.

Vita hiyo imeibuka, kufuatia msukumo wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ukraine, Mykhaylo Fomenko wa kutaka mshambuliaji huyo kucheza ligi kuu ya soka nchini England ili kujiongezea uwezo wa kupambana kikamilifu anapokua uwanjani.

Fomenko aliwaambia waandishi wa habari kwamba, anafurahishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo, lakini anaamini atafurahi zaidi kama atapata nafasi ya kucheza ligi yenye ushindani kama ya England.

“Kama anahotaji kujiendeleza na kuwa mshambuliaji mwenye uzoefu mkubwa, ninamshauri akacheze nchini England ambapo kila leo pamekua na ushindani wa hali ya juu.” Fomenko aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Ukraine dhidi ya Wales.

“Ni kiongozi mzuri wa kikosi changu, na ningependa kuendelea kumuona akiendelea kuwaongoza wengine kama mfano wa kuigwa.” Aliongeza kocha huyo

Tayari uongozi wa klabu ya Dynamo Kiev, umeshamuweka sokoni mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kiasi cha pauni million 25.

Mwezi januari mwaka huu, Arsenal walitajwa kuwa katika mipango ya kumsajili Yarmolenko, lakini ilishindikana kutokana na klabu yake kumuhitaji katika michuiano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, lakini itakapofika mwishoni mwa msimu huu, atakua huru kuondoka.

Yarmolenko alifunga bao la ushindi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Ukraine dhidi ya Wales uliochezwa mwanzoni mwa juma hili.

Watu 7 Wauawa Ajali ya Ndege Canada
Unyama: Mwanamke amchinja na kumnyofoa moyo mpenzi wake kwa kosa hili