Zikiwa zimebaki siku 4 watanzania wamchague Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amewataka wananchi kutomchagua mgombea wa CCM, Dkt. Magufuli.

Bi. Mgwira aliotoa kauli hizo jana alipokuwa akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Mugumu mkoani Mara na kudai kuwa serikali ya CCM imegawa bure fulana, kofia na kusomba wananchi kwa malori  wakitumia kiasi kikubwa cha fedha wakati watoto wanakaa chini mashuleni na hawapati vyakula.

 “Sasa hivi tisheti za njano na kofia zimetapakaa sana, wanagawa bure na kusomba watu kwa malori ili wajae kwenye mikutano yao, wakati watoto wanakaa chini, hawapati chakula shuleni, watumishi hawalipwi, dawa hospitali hakuna, barabara mbovu ni kipindi cha kuwataka wapishe Ikulu. Kwa zaidi ya miaka 15 wanahaidi tu, wilaya hii yenye neema na jina kubwa ndio imesahaulika hivi? wanathamini wanyama kuliko watu, muikatae CCM mwaka huu.”

Joe Biden Amuondolea Kikwazo Hillary Clinton, Urais Wa Marekani
Ashley Young Aachwa Old Trafford