Makamu wa Rais wa Marekani, Joseph ‘Joe’ Biden alitangaza rasmi jana kuwa hatawania urais mwaka 2016, hivyo, kuondoa kikwazo kwa Hillary Clinton katika upande wa Democratic kwa kuwa ndiye aliyekuwa mshindani wake mkuu.

Joe Biden ametangaza uamuzi huo ndani ya Ikulu ya Marekani, Rose Garden akiwa na rais Barack Obama pembeni yake pamoja na mkewe, Dkt. Jill Biden. Alisema kuwa mwanzoni familia yake iliweza kuyavumilia maumivu ya kuondokewa kwa mwanae mkubwa wa kiume na kuona wanaweza kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi, lakini siku kadri siku zilivyokuwa zinaenda hadi kufikia siku ya ukomo wa kurejesha fomu, aliamua kuwa hakuwa tayari kugombea tena.

Rais Obama akimuangalia Joe Bidden aliyemgeukia Mkewe, Dkt. Jill Biden baada ya kutoa hotuba yake

Rais Obama akimuangalia Joe Bidden aliyemgeukia Mkewe, Dkt. Jill Biden baada ya kutoa hotuba yake

“Bahati mbaya naamini tukko nyuma ya wakati muhimu wa kushinda kampeni za kura za maoni. Lakini wakati ambapo sitakuwa mgombea, sitakuwa kimya,” alisema Joe Bieden.

Aidha, alisema litakuwa kosa kubwa kwa mtu yeyote katika chama cha Democratic kutotambua rekodi nzuri ya utendaji iliyowekwa na Rais Barack Obama.

Video: Lowassa Ajibu Kuhusu Afya Yake, Atakachofanya Endapo Atashindwa, Elimu Bure Na Mengine
Anna Mghwira ampiga kikumbo Magufuli