Mwenyekiti wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Anna Mghwira amelaani usaliti uliofanywa na aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama hicho, Khamis Idd Lila dhidi ya chama hicho kwa kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho kuhusu uchaguzi wa marudio.

Bi. Mghwira ambaye alikuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia chama hicho ameiambia EATV kuwa chama chake tayari kilishatoa msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi na kwamba hata mgombea huyo alikuwa mmoja kati ya waliopitisha msimamo huo hapo awali.

“Sijui ni nini tena kimemsukuma kuchukua uamuzi huo na kutangaza tena kuwa atashiriki katika uchaguzi wa marudio,” alisema Mghwira.

Alisema kuwa msimamo wa chama hicho wa awali ulikuwa kupinga uchaguzi wa marudio lalini kwa sasa ni kutoshiriki uchaguzi wa marudio kwani hauzuiliki tena.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya wagombea kwenye uchaguzi huo wa marudioa kwani hakuna mgombea yoyote aliyefuata utaratibu wa kisheria wa kujitoa.

 

 

Uingereza yamwagia sifa Magufuli, yaahidi haya
Himid Mao Kuikosa Tanzania Prisons J’5