Wachezaji wa safu ya kiungo  wa Arsenal Mesut Ozil na Aaron Ramsey pamoja na kipa Petr Cech watarudi katika mechi ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya mabingwa watetezi Barcelona usiku wa leo.

Wachezaji hao walipumzishwa katika mechi ya kombe la FA siku ya Jumamosi dhidi ya Hull City.

Barca itamrudisha katika kikosi chake beki Gerard Pique, ambaye alipumzishwa katika ushindi dhidi ya Las Palmas na kiungo wa kati Sergio Busquets ambaye alikuwa akihudumia marufuku.

”Tunahitaji kuwa na mwelekeo katika mechi hiyo kwa pamoja ili kuwa na fursa ,”alisema mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger.

Arsenal iliondolewa na kilabu ya Monaco katika mchujo wa msimu uliopita.

Walipoteza kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Emirates,lakini wakashindwa kufuzu baada ya kushinda maba 2-0 ugenini kutokana na bao la ugenini.

”Ni fursa kuonyesha kwamba tumepata funzo,kwa sababu tulijipatia kibarua kigumu baada ya mechi ya nyumbani,”alisema.

Kazimoto Aomba Msaada Wa Wakili
Malinzi: Mwenye Ushahidi Aupeleke TAKUKURU