Kiungo kutoka nchini England na klabu ya Arsenal, Alex Oxlade Chamberlain atakuwa nje ya uwanja kwa majuma madhaa yajayo kutokana maumivu ya goti yanayomkabili.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 alipatwa na maumivu ya goti, wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya FC Barcelona uliochezwa usiku wa kuamkia siku ya jumatano.

Chamberlain, aliumia goti alipokabiliana na kiungo wa FC Barcelona Javier Mascherano, hali ambayo ilimsababishia ondoke uwanjani akiwa na usaidizi wa kutembelea magongo.

Wenger amesema jeraha la kiungo huyo, limeshindwa kupatiwa ufumbuzi wa muda wa kupona kwake na badala yake wanakadiria huenda likamchukua muda wa majuma manne mpaka sita.

Spurs Wapewa Ruhusa Ya Kujenga Uwanja Jijini London
Magufuli awapa saa nne mawaziri wake, vinginevyo watakuwa wamejitumbua jipu