Washika bunduki wa Ashburton Grove (Arsenal) wamepiga hatua katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania, Alvaro Morata ambaye juma lililopita alithibishwa kurejea mjini Madrid.

Arsenal wanatajwa kupiga hatua kubwa za usajili wa mshambuliaji huyo, tofauti na ilivyo kwa Chelsea ambao pia wana hamu ya kuona Morata anatua Stamford Bridge.

Tayari mshambuliaji huyo ameshaeleza wazi mipango ya kutaka kucheza soka lake nchini England, baada ya kurejea Real Madrid akitokea Juventus kama mkataba wake ulivyokua unaelekeza.

Arsenal wamedai kuwa tayari kutoa dau la Pauni milioni 65 linalotakiwa na Real Madrid ili kukamilisha usajili wa Morata, lakini mpaka sasa Chelsea hawajazungumza lolote kuhusu kukubali ama kukataa kuhusu mchakato wa suala hilo.

Endapo dili hilo litakamilishwa kama linavyotarajiwa, Real Madrid wataingiza faida kubwa ya kipesa, kufuatia baadhi ya vifungu vya mkataba wa Morata kueleza kwamba alipaswa kurejeshwa klabuni hapo kwanza, pale dili la usajili litakapojitokeza.

Morata alikua sehemu ya kikosi cha Hispania kilichoshiriki fainali za Euro 2016 zinazoendelea nchini Ufaransa na alifanikiwa kufunga mabao matatu.

Ahmed Musa Kuhalalishwa Mwishoni Mwa Juma Hili
Mancini Kuingia Kwenye Kinyang'anyiro cha Ukocha Wa England?