Mabingwa wa soka nchini England, Leicester City watathibitisha kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Nigeria na klabu ya CSKA Moscow, Ahmed Musa mwishoni mwa juma hili.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alipangiwa kufanyiwa vipimo vya afya jana, lakini taarifa za kukamilisha mpango huo hazikusikika na haijaeleweka kwa nini ilifanywa kuwa siri.

Baada ya mpango huo, Leicester City walipaswa kuwasilisha fedha za usajili wa mshambuliaji huyo, ambazo zinakadiriwa kufikia Pauni milioni 18, kwenda katika klabu ya CSKA Moscow ya nchini Urusi.

Kutokana na ukimya uliotawala, tovuti na klabu ya Leicester City imeeleza kwamba kuna uwezekano wa suala la mshambuliaji huyo likakamilishwa mwisihoni mwa juma hili, pasi na kificho chochote.

Claudio Ranieri ameonyesha kuvutiwa na mshambuliaji huyo, kutokana na juhudi zake zilizowezesha mafanikio ya klabu ya CSKA Moscow kwa kufunga mabao 50 tangu aliposajiliwa mwaka 2012, akitokea kwenye klabu ya VVV-Venlo ya nchini Uholanzi.

Mapambano yaendelea Sudani Kusini
Arsenal Waonyesha Dhamira Ya kweli Kwa Alvaro Morata