Watu wapatao laki mbili nusu wamehama makazi yao  na kwenda kwenye maeneo salama ambayo ni karibu na kambi ya vikosi vya umoja wa mataifa.

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini kimesema kwamba kumekuwa na milio ya risasi zaidi katika mji wa kaskazini magharibi wa Wau.

Serikali ya Sudan imesema kwamba wiki iliyopita watu 43 walifariki walipokuwa katika mapambano kwenye mji huo wa Wau, wakati huo raia wanasema idadi ni kubwa kuliko inavyoelezwa

Mapambano hayo yanatoa taswira iliyodhahiri kwamba hali ya amani bado haijatengamaa Sudan Kusini,siku mbili kabla kulikuwa na maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru wa nchi hiyo kama taifa huru.

Hata hivyo wakati hayo yakiendelea  imeripotiwa mapigano mengine katika mji mkuu wa Juba ambapo magari ya kijeshi yalifunga barabara mashuhuda waliliambia shirika la habari la Reuters.

BBC

Video: Mambo 6 yanayomhusu Cristiano Ronaldo
Ahmed Musa Kuhalalishwa Mwishoni Mwa Juma Hili