Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemjibu gwiji wa soka nchini Nigeria Austin Jay Jay Okocha, ambaye alionyesha kutopendezwa na mpango wa mpwa wake Alex Iwobi kukalishwa benchi huko kaskazini mwa jijini London.

Juma lililopita Okocha alidai kuwa, Iwobi yupo hatarini kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza, baada ya kuakalishwa benchi katika michezo mitatu iliyopita ambayo iliihusisha Arsenal.

Wenger amewaambia waandishi wa habari kuwa, kukosekana kwa Iwobi katika michezo mitatu iliyopita kunatokana na kubadilika kwa mfumo wa uchezaji klabuni hapo ambao umewafanya wachezaji kama Theo Walcott na wengine wengi wajikute wakiwa nje ya kikosi cha kwanza.

Kwa sasa Arsenal inatumia mfumo mpya wa 3-5-2 kutoka ule wa zamani wa 4-3-3.

 

Meya wa Jiji la Dar ahudhuria mkutano wa majiji nchini Iran
TRA yajidhatiti katika ukusanyaji mapato