Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekiri kuwa yuko sokoni akisaka nyota wapya katika dirisha dogo la usajili huku akidai kwamba anahitaji kufanya mageuzi katika kikosi chake.

Alisema lengo lake ni kuhakikisha timu yake inaimarika zaidi na kulinda matokeo mazuri waliyoyavuna katika nusu ya kwanza ya msimu huku wakiwa kileleni mwa Premier League.

“Nataka kubadili mfumo wa washambuliaji wangu wasipoteze nafasi za kupachika mabao, tumekuwa tukipoteza nafasi nyingi,” alisema Wenger

Wakati Arsenal ikiaminika kuwa tayari imemnasa kiungo Mohamed Elneny wa Basle, klabu hiyo pia inahusishwa na usajili wa winga wa  Leicester City, Riyad Mahrez.

Basle defensive midfielder Mohamed Elneny is set to sign for Arsenal in a £7.4m deal in JanuaryKiungo mkabaji  wa Basle  Mohamed Elneny anatarajiwa kutua Arsenal kwa pauni milioni 7.4 katika usajili wa Januari

Bojan Kuwindwa Kwa Udi Na Uvumba Januari 2016
Lionel Messi Acheza Game Ya 500 Akiwa Barcelona