Meneja wa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa jijini London *Arsenal*, Mikel Arteta, amethibitisha kiungo kutoka nchini Uswiz Granit Xhaka ataendelea kusalia klabuni hapo kwa msimu ujao 2021/21.

Arteta ametoa ufafanuzi huo, kufuatia Xhaka kuhusishwa na taarifa za kutaka kuihama Arsenal katika kipindi hiki cha dirisha la usajili.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amesema Xhaka bado ni kiungo muhimu kikosini kwake, na anamuhitaji kwa mipango ya msimu ujao utakaoanza hivi karibuni.

Katika hatua nyingine Arteta amesema Arsenal imempa ofa kiungo huyo ya kusaini mkataba mpya wa hadi Juni 2025, kwa kumuahidi kumuongezea mshahara kwa mkataba huo mpya atakaosaini.

Arsenal inaamini itakamilisha mazungumzo hayo dhidi ya nyota huyo hivi karibuni, hii ni baada ya kukataa ofa ya Pauni Milioni 12 na nyongeza ya Pauni Milioni 3 kutoka Klabu ya AS Roma ya Italia, iliyokuwa inahitaji saini ya nyota huyo.

Mtibwa Sugar kumsajili Said Makapu
UCHAMBUZI: Kocha Lwandamina hana la kujitetea